WASHINGTON, MAREKANI
RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema katika bajeti ya mwaka 2018 atapunguza matumizi ya ndani kwa ajili ya kujenga jeshi la nchi hiyo
Baadhi ya wataalamu wa uchumi wamemshangilia Trump wakati wanachama wa chama chake wanahofia kuwa bajeti hiyo italazimisha kupunguza miradi maarufu mbalimbali kama misaada kwa watoto walemavu na chakula kwa ajili ya wazee.
Wengine, wakiwa ni pamoja na wanachama wa Freedom Caucus, wanasema bajeti siyo rahisi kama inavyosema.
Ikulu ya Marekani imetoa maelezo machache kuhusiana na bajeti ya Trump na kusema rais anataka kuongeza nguvu ya jeshi kwa dola za Marekani bilioni 54 na anatafuta maeneo mengine ya kupunguza matumizi katika miradi isiyo ya ulinzi.