27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DC:MLIOFICHA POMBE ZA  VIROBA JISALIMISHENI

Na ELIUD NGONDO, CHUNYA


MKUU wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, Rehema Madusa amewataka wafanyabiashara walioficha pombe kali aina ya viroba vilivyopigwa marufuku na Serikali wahakikishe wanajisalimisha mapema ili kunusuru kukamatwa na mkono wa Serikali.

Rehema, aliyasema hayo jana mji mdogo wa Makongolosi ambako kulifanyika  msako wa wafanyabiashara hao na kufanikiwa kukamata baadhi yao wakiwa na  pombe hizo.

Madusa aliwataja, waliokamatwa kuwa ni Nestory Filbert (23) mkazi wa Lupatingatinga akiwa na paketi 9,849 aina ya Shujaa na paketi 100 za Konyagi na  Jackson Elias (55) mkazi wa Makongolosi akiwa viroba paketi 225 aina mbalimbali.

Mfanyabiashara mwingine, ni Filbert Kalumanzila (60)mkazi wa Makongolosi ambaye alikuwa na paketi 240 aina ya Ridder zinazotoka nchini Malawi na Joshua Mwakaja (42) mkazi wa Makongolosi akiwa paketi 100 aina ya Ridder,Gun 165 na chupa za Ridder 60.

Alisema mtuhumiwa mwingine, Joyce Bathlomeo (36) mkazi wa Kibaoni,alikamtwa akiwa na viroba vya aina mbalimbali ambavyo ni “high life” paketi 180 na aina ya Fiesta paketi 450, zikiwa zinauzwa katika duka lake la jumla.

“Pombe zilizo kamatwa ni aina nyingi sana zingine, ni Van Roh, Leader’s, Players, Kahawa Fusio, Double Punch, Charger Tanzania, Bwenzi, Rider na watuhumiwa watachukuliwa hatua za kisheria.” alisema Madusa.

Joshua Mwaisenye, mkazi Makongolosi alisema wafanyabiashara wanatakiwa kuzingatia maagizo Serikali juu ya ukatazwaji wa kutumia pombe kali ambazo zimekuwa na madhara makubwa kwa vijana.

Alisema pombe hizo, zimekuwa zikitoka nchi za Zambia na Malawi na kuingizwa nchini na kuongeza madhara makubwa kwa vijana.

Naye Alex Kinyamagoha, alisema viroba hivyo vinavyo ingizwa nchi vina ujazo wa asilimia 43 kwa paketi moja.

“Tumewahi kushuhudia wenzetu vijana wakipoteza maisha kutokana na unyaji wa hizi,zimekuwa zikitoka nchi za Malawi na Zambia zinaingizwa kwa njia ya panya,” alisema Kinyamagoha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles