32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

JK AFURAHIA MAISHA YA URAIANI

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, alisema kwa sasa amepumzika na anafurahia maisha ya kustaafu.

“Nimepumzika na-enjoy (nafurahia) maisha ya kustaafu,” alisema Rais Kikwete na kushangiliwa.

Kuhusu mabadiliko hayo alisema yataongeza ufanisi katika chama hicho na kuwataka wanachama kutokuwa na hofu.

“Mwaka juzi nilikukabidhi (anamweleza Rais Dk. Magufuli) ‘mabook’ mawili ya tathmini tuliyofanya, wakati mwingine ukipigwa madongo pole bwana pengine ningepigwa mie…wewe ndiye uliopo,” alisema Rais Kikwete.

Alisema mabadiliko hayo yatasaidia chama hicho kuweza kujiendesha ikizingatiwa changamoto mojawapo ya chama hicho ni   gharama kubwa za uendeshaji huku vyanzo vyake vya mapato vikiwa ni ada za uanachama na kuuza mali za chama.

“Tuna wanachama milioni nane, kama wote wangekuwa wanalipa ada tungekuwa na uhakika wa Sh bilioni 12 na kungekuwa hakuna cha kutuhangaisha tukiongeza na ruzuku zetu.

“Lakini kwenye ada unakuta tunapata Sh milioni 500 tu, gharama za mkutano wa halmashauri kuu ya taifa ni Sh milioni 600, hivyo lazima rais ahangaike kusaidia,” alisema   Kikwete.

Pia alimpongeza Katibu Mkuu wa Chama hicho, Kinana kwa kazi nzuri anayoifanya na kusema kuwa anastahili kutambuliwa.

“Tungekuwa hatuna Katibu Mkuu kama Kinana hali yetu ingekuwa ngumu sana, anastahili kutambuliwa,” alisema.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi, alizungumza kwa kifupi   aliyafananisha mabadiliko ya chama hicho sawa na tsunami.

MWINYI   

Mwinyi ndiye aliyekuwa wa kwanza kupewa nafasi ya kuzungumza na Rais Dk. Magufuli baada ya kumaliza kuendesha hatua ya kupiga kura ya mabadiliko ya katiba ya chama hicho.

“Nakushukuru Mwenyekiti kwa kunipa nafasi hii…haya ni mabadiliko ya tsunami,” alisema Mwinyi.

DK. SHEIN

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein, aliwaasa wanachama wa chama hicho kujenga utaratibu wa kuipitia katiba  kujua kanuni zake na maadili ya chama.

“Tukawatumikie wana- CCM na Watanzania wote bila ubaguzi wowote,” alisema Dk. Shein.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles