30.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

UPINZANI: TUTAWASHUGHULIKIA AKINA KENYATTA KWA UFISADI

MOMBASA, KENYA


KINARA mwenza wa Muungano wa Upinzani (NASA) Musalia Mudavadi, juzi alisema Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto watawajibika kwa kashfa za ufisadi zilizotokea chini ya utawala wao, iwapo upinzani utashinda Uchaguzi Mkuu wa Agosti, mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika eneo la Mikindani kaunti Mombasa, Mudavadi alisema Kiongozi wa wengi Bungeni, Aden Duale na aliyekuwa Waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru pia watajibu maswali kuhusu kashfa za ufisadi.

“Watalazimishwa kuwaeleza Wakenya kuhusu kashfa za wizi wa mabilioni ya fedha katika Shirika la Vijana kwa Huduma za Taifa (NYS) na zile zilizokutokana na mauzo ya hati za dhamana katika masoko ya ng’ambo, Eurobond.

Kiongozi huyo wa Chama cha Amani National Congress (ANC) alisema viongozi wa Jubilee pia watawajibika kwa ubadhilifu wa mabilioni ya fedha zilizotumika kufadhili miradi mikubwa ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

“Wanataka kusalia mamlakani ili wasiwajibishwe,” Mudavadi, ambaye umaarufu wake wa kisiasa umekuwa ukipanda chini ya mwavuli wa NASA alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles