25.6 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

WALIMU WATAKIWA KUWA WABUNIFU

NA ASHA BANI-Dar es Salaam


TAASISI isiyo ya Serikali ya Techers Junction, imewashauri walimu wote nchini kuwa wabunifu wapate mbinu bora za kuweza kufundisha wanafunzi.

Wito huo ulitolewa Dar es Salaam jana, wakati baadhi ya walimu wakipatiwa mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo wa kufundisha wanafunzi darasani.

Akitoa mafunzo hayo, Ofisa Mradi wa taasisi hiyo, Njama Salum, alisema walimu wanapomaliza vyuo mbalimbali wanatakiwa kuwa na uwezo wa kubuni njia za kufundishia zitakazomfanya mwanafunzi kuwa na nguzo imara ya kuendelea kufanya vizuri shuleni.

Alisema licha ya walimu kuwa na changamoto mbalimbali, bado wanatakiwa kuendelea na mbinu za kutoa ujuzi vichwani mwao na kuupeleka ujumbe huo wa elimu vichwani mwa wanafunzi kuwawezesha kufanya vizuri.

“Tunafahamu changamoto ni nyingi kwa walimu, lakini hata kwa wale waliopata nafasi za kufundisha ni vema wakawa na mbinu nzuri za ufundishaji, ikiwa ni pamoja na mwalimu kusimama wakati anafundisha na kuhakikisha anamfikia mwanafunzi kwa ufasaha zaidi,’’ alisema Salum.

Alisema taasisi hiyo imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia walimu kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo ya mbinu za ufundishaji, kuwapa misingi bora ya ualimu na kutoa ushauri mzuri utakaowajenga walimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles