26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MAKALLA ATOA SIKU 14 KUPIMA MIPAKA

Na ELIUD NGONDO, MBEYA


Amos-Makala-600x330MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, amewaagiza maofisa ardhi, wapimaji ramani kufanya kazi ya kupima mpaka wa Kijiji cha Kapunga na Ukwavila kwa muda wa siku 14 ili kutatua mgogoro uliodumu miaka 10.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati wa  mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi katika Kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali, ambapo wananchi walilalamika kutoelewana kutokana na uongozi wa vijiji  kuwapa wawekezaji maeneo yao.

Makalla alisema katika vijiji hivyo kumekuwapo na mgogoro ambao umekuwa ni kero kutokana na wawekezaji kuwekeza katika mashamba ya wananchi, huku wazawa wakiwa hawana mashamba.

Alisema maofisa wa upimaji kutoka  mkoani wafanye kazi hiyo ili kutambua mpaka wa vijiji hivyo viwili na baada ya hapo atatoa uamuzi.

“Maofisa wa upimaji kutoka ofisini kwangu watakuja kupima tena kazi hii, itachukua  siku 14 na baada ya kupima na wakaniletea jibu, mimi nitakuja sasa kutoa uamuzi, kuna watu wataupenda na wengine watauchukia,” alisema Makalla.

“Nasikia  hamuwaamini wapimaji  kutoka ngazi ya wilaya, wapimaji kutoka ngazi ya mkoa wanakuwa  hapa na watafanya kazi hii kwa muda  huo niliousema, kama hamtaki kuwaamini hata wakija watu kutoka wizarani napo mtasema hamuwaamini, sasa jibu watakalolileta ndilo litakuwa ni uamuzi,” alisema Makalla.

Kwa upande wao, wananchi walisema mgogoro huo umekuwa ukisababishwa na viongozi wa vijiji kwa kuwamilikisha wafanyabiashara wakubwa mashamba kinyume na utaratibu unavyotakiwa.

Mkazi wa Kapunga, Suleiman Kapalamba, alisema mgogoro huo umekuwa ukichochewa zaidi na wawekezaji ambao wamepewa maeneo makubwa na wananchi wakiwa hawana sehemu za kulima.

Naye Iyasa Mgaya, alisema katika migogoro ya Kijiji cha Ukwavila na Kapunga haihusishi kaya kwa kaya, bali wawekezaji ndio wamekuwa  tatizo kubwa kwa kusababisha kutokuwepo na kuelewana.

Alisema wamekuwa na tamaa ya kuchukua fedha kutoka kwa wawekezaji na kuwapa mashamba bila kufuata utaratibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles