25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

WAJAWAZITO WAENDA NA MAJI KUJIFUNGUA

Na SAFINA SARWATT- MOSHI


ujauzitoZAHANATI ya Kijiji cha Mandaka Mnono, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji safi na salama.

Kutokana na hali hiyo, wanawake wanaokwenda katika zahanati hiyo kujifungua, wamekuwa wakienda na ndoo za maji kutoka nyumbani kwao.

Hayo yameelezwa juzi na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto, Wilaya ya Moshi, Elvast Mshana, wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho
kuhusu athari zinazotokana na ukosefu wa maji katika zahanati hiyo.

“Kwa sasa huduma za afya zinazotolewa katika zahanati hiyo si za kuridhisha kwa sababu hakuna maji na jambo hili limekuwa kero kwa wajawazito wanaokwenda kujifungua.

“Ninachokiona mimi ni kwamba ni bora sasa wananchi mkafanya utaratibu wa kuhakikisha  maji yanapatikana kwa sababu tatizo hili limekuja baada ya pampu ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni saba kuibiwa,” alisema Mshana.

Naye mkazi wa kijiji hicho, Bangaiza Mkonyi, aliilalamikia halmashauri ya wilaya yao na kusema imeshindwa kununua pampu mpya na kuwafanya wananchi wa kijiji hicho kupata shida.

“Pamoja na kwamba tunapata shida ya maji kwa sababu ya kuibiwa kwa pampu ya maji, lakini ieleweke kwamba tatizo hilo lilisababishwa na halmashauri kwa sababu ilimhamisha ofisa mtendaji wa kata wakati kuna upotevu wa pampu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles