Urusi imeonya kulipiza kisasi hatua ya rais wa Marekani Barrack Obama ya kuwatimua wanadiplomaisa 35 wa Urusi kufuatia tuhuma kwamba Urusi iliingilia maswala ya uchaguzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa mitandaoni.
Msemaji wa rais Vladmir Putin amesema kuwa hatua zitakazochukuliwa na Urusi zitaiathiri Marekani na pamoja na mambo mengine, Urusi pia imesema itawafukuza wanadiplosmasia 35 Warekani na
Kwa mujibu wa Rais Obama, amesema Urusi pia imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani.
Kwa upande wake, rais mteule Donald Trump ambae mara kwa mara amekuwa akizipuuzilia taarifa hizo za udukuzi, sasa amesema atakutana na wakuu wa kiintellijensia wa Marekani ili kupata undani zaidi wa swala hilo.
Awali, Rais Obama aliamuru kutimuliwa kwa wanadiplomaisa 35 wa Urusi kufuatia tuhuma za Urusi kutaka kuingilia kati uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao.
Lakini pia makazi ya wanadiplomasia wawili wa Urusi yamefungwa na baadae kuwekewa vikwazo.
Obama ameendelea kusema wamarekani wote sharti washtushwe na vitendo vya Urusi, hii ikionekana kama njia ya kumjibu mrithi wake Donald Trump ambae amesema kila mtu aishi maisha yake.