32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Bunge kuanza leo mjini Dodoma

job-ndugaiNa SARAH MOSES ,DODOMA

MKUTANO wa tano wa Bungela la 11 unaanza leo mjini hapa huku Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba tatu ya mwaka 2016 ikitarajiwa kujadiliwa.

Pia katika mkutano huo wabunge wanatarajia kupata angalau siku moja kwa ajili ya kujadili mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na Jumuiya ya Ulaya kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema mkutano huo unafuatiwa na vikao vilivyokuwa vikiendelea kwa wiki mbili mjini hapa, ambapo kamati za Bunge zilikutana na kujadili mambo mbalimbali .

Ndugai alibainisha kuwa mkutano huo unaoanza leo shughuli yake ya kwanza inaongozwa na kanuni ya 94  ambapo inatakiwa mkutano wa Oktoba/ Novemba pamoja na mambo mengine ukae kama kamati ya mipango ili ujadili, kupokea na kutoa maoni kuhusiana na  mwongozo wa kuandaa bajeti ijayo ya Serikali.

“Kupitia mjadala huu tunatarajia kwamba serikali itapata ushauri kuhusu vyanzo mbalimbali vya mapato, kama maeneo fulani kuna sehemu ya kuongeza au kupunguza kwa maana ya bajeti inayokuja”alisema Ndugai.

Alisema pia kupitia mjadala huo wanatarajia kupata ushauri kuhusiana na vipaumbele ambavyo ni vema vikatiliwa mkazo katika bajeti inayokuja ya mwaka 2017/2018.

“Kutakuwa na kipindi cha maswali na majibu kama kawaida ambapo kutakuwa na maswali 215 yakifuatiwa na maswali yasiyozidi kumi siku ya alhamisi,” alisema Ndugai.

Alisema katika mkutano huo kutakuwa na taarifa ya CAG na majibu ya serikali kuhusiana na taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles