25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Babu Tale: Diamond hajapokea fedha za Lowassa

f03aa272bfLNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

MENEJA wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amesema hawajawahi kupewa kiasi cha fedha Sh mil 500 na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili wampigie kampeni za urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na MTANZANIA hivi karibuni, Babu Tale alisema watakuwa wehu kukataa fedha nyingi kiasi hicho wakati wenyewe wanafanya muziki ili kupata fedha, lakini ukweli ni kwamba hawajapewa kitu chochote.
Alisema hata hivyo Diamond yupo tayari kumfanyia kampeni mgombea yeyote atakayetangazwa kuiwakilisha CCM. “Kama kweli tungekataa fedha hizo hata Mwenyezi Mungu angetulaani, ila naamini taarifa hizo zitakuwa zinasambazwa na wapinzani wa kisiasa wa kiongozi huyo, hatujawahi kutupa ofa hiyo,” alisema Babu Tale.
Meneja huyo alitoa ufafanuzi huo baada ya hivi karibuni kuzagaa kwa taarifa ambazo si za kweli, kwamba walipokea kiasi hicho ili kumpigia kampeni Lowassa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles