Viongozi wa Vyuo Vikuu Dar es salaam wanataraji kufanya ziara ya kutembelea nyumba aliowahi kuishi Hayati Mwl Julius Nyerere iliyopo Magomeni jijini hapa.
Kwa mujibu wa Mratibu wa ziara hiyo, Marco Bujiba, amesema lengo la ziara hiyo ni kutafakari kwa upana juhudi za Baba wa Taifa kulikomboa Taifa kwa kupambana na umaskini, ujinga na maradhi.