24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Lipumba akataliwa Tanga

lipumbaNa AMINA OMARI, TANGA

WAKATI Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, akikamilisha ziara katika mikoa ya Mtwara na Lindi, viongozi wa chama hicho wa Mkoa wa Tanga, hawatampa ushirikiano kama akianza ziara mkoani humo keshokutwa.

Taarifa hiyo imetolewa juzi na Mwenyekiti wa Chama hicho, Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Jumbe alitoa msimamo huo wakati Profesa Lipumba akitarajiwa kuanza ziara hiyo ya kukiimarisha chama katika Wilaya za Muheza na Korogwe, mkoani hapa.

“Sisi hatutambui ziara hiyo na hatutashiriki kwa sababu yeye si mwenyekiti wa chama chetu kwani alishafukuzwa uanachama na baraza kuu la chama chetu.

“Kwa hiyo, narudia tena hatutashirikiana naye kwa namna yoyote ile, kwa sababu mgogoro aliouanzisha katika chama unaonyesha ni kwa jinsi gani anavyotaka kukidhoofisha chama.

“Hivyo basi, viongozi watakaoshiriki katika mapokezi pamoja na ziara hiyo katika wilaya husika, watakuwa wamekiuka miongozo, taratibu pamoja na kununi za chama,” alisema Jumbe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Uhamasishaji wa Jumuiya ya Wazee wa CUF, Omari Ally, aliwataka wafuasi wa chama hicho kutoshirikiana na Profesa Lipumba kwa kuwa ana nia ya kukidhoofisha chama chao.

Pamoja na hayo, alionyesha kutoridhishwa na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, aliyekaririwa hivi karibuni kwamba anamtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti wa chama hicho.

“Msajili wa vyama vya siasa hana mamlaka ya kuwachagulia viongozi vyama vya siasa. Kwa hiyo, kitendo kilichofanywa na msajili huyo ni kinyume kabisa na taratibu, kanuni na sheria za nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles