29.4 C
Dar es Salaam
Saturday, December 14, 2024

Contact us: [email protected]

Akina Kitilya bado wasota korokoroni

kitillyNa MANENO SELANYIKA – DAR ES SALAAM

UPELELEZI wa kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wawili bado haujakamilika.

Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba.

Wakili wa Serikali, Estazia Wilson, alidai mahakamani kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa, aliomba upande wa Jamhuri uharakishe kukamilisha upelelezi kwa sababu wateja wake wamekaa mahabusu kipindi kirefu.

Baada ya kusikiliza pande hizo mbili, Hakimu Simba ilipanga kesi kutajwa tena mahakamani hapo Oktoba 21 mwaka huu na kuamuru washtakiwa kurejeshwa mahabusu.

Katika kesi ya msingi, Kitilya, aliyekuwa Miss Tanzania 1996, Shose Sinare na aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Limited, Sioi Solomon, wanashtakiwa kwa makosa ya utakatishaji wa fedha, kutumia nyaraka za kughushi na za uongo na kujiptia Dola za Marekani milioni 6, sawa na Sh bilioni 12 kinyume cha sheria.

Pia ilidaiwa mahakamani kuwa tarehe tofauti, kati ya Agosti 2012 na Machi 2013 jijini Dar es Salaam, washtakiwa walipanga kwa ushirikiano na watu wengine kujipatia fedha kutoka serikalini kwa njia ya udanganyifu.

Kwamba Agosti 2, 2012 katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki ya Stanbic Tanzania Limited zilizopo Kinondoni, Sinare akiwa na nia ovu alighushi taarifa za maombi ya fedha katika Benki ya Standard.

Washtakiwa walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Aprili mosi mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles