Na MASANJA MABULA, WETE
ABIRIA 101 waliokuwa wakisafiri kutoka Kisiwani Pemba kwenda Tanga kupitia Bandari ya Wete, wamekwama bandarini.
Abiria hao wamekwama mahali hapo baada ya nahodha na mabaharia wa mashua waliyokuwa wakisafiria, kukamatwa.
Nahodha wa mashua hiyo, Â Â Badili Tabia yenye namba za usajili, Z 158, ilikuwa ikiongozwa na nahodha, Daud Mkashari Mpemba.
Taarifa zilizopatikana zinasema   nahodha na mabaharia hao 13 walikamatwa kwa kuwa walikiuka agizo la Serikali la kuzuia mashua kusafirisha abiria.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, agizo la kukamatwa nahodha na mabaharia hao lilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wilaya ya Wete, Abeid Juma Ali baada ya kufanya ziara ya kushitukiza bandarani hapo na kukuta mashua hiyo ikiwa imepakia abiria.
Pamoja na kuzuia safari hiyo, Ali alisema abiria hao hawakuwa wameorodheshwa majina yao katika maeneo husika, jambo ambalo  lingeleta utata kama wangepata matatizo safarini.
“Uamuzi wa Serikali kuzuia mashua kusafirisha abira ni kulinda usalama wao kwa vile  vimesajiliwa kwa ajili ya kubeba mizigo.