27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

Jela miaka saba kwa kumng’oa meno mwanawe

tooth-extraction

Na FARAJA MASINDE, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, imemhukumu miaka saba jela na viboko 12, mwanamume mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga na kumng’oa meno mtoto wake.

Mshtakiwa huyo, Elisha Sumila (35), ambaye ni mkulima na mkazi wa Ukonga alihukumiwa jana na Hakimu Mkazi, John Msafiri baada ya kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka.

Katika ushahidi huo uliomtia hatiani mshtakiwa huyo, kulikuwa na mashahidi sita na vielelezo vitatu kikiwamo cha daktari.

“Kulingana na kosa ulilofanya na Mahakama hii kwa kuzingatia hoja zilizowasilishwa na upande wa mashtaka inakutia hatiani kutumikia kifungo cha miaka saba jela.

“Pamoja na kifungo hicho pia utachapwa viboko 12, sita unapoingia na sita unapotoka iwe onyo na fundisho kwa wazazi wenye tabia kama hii,” alisema Hakimu Msafiri.

Awali ilidaiwa na Wakili wa serikali, Sylvia Mitanto   kuwa hakukuwa na kumbukumbu za mashtaka ya nyuma dhidi ya mshtakiwa na hivyo kuiomba kutoa adhabu kali.

“Mtuhumiwa amemsababishia mwanawe huyo wa kumzaa ulemavu wa kudumu bila sababu, hivyo naomba mahakama impe adhabu kali ambayo itamfanya ajutie na kuwa fundisho kwa wazazi wote wenye tabia kama hizi za kunyanyasa watoto,” alisema Wakili Mitanto.

Katika kesi hiyo namba 257 ya mwaka 2014, inadaiwa kuwa Agosti 28 mwaka juzi maeneo ya Ukonga Mazizini, Manispaa ya Ilala, Sumila alimpiga mtoto wake, Aman Sumila, kumng’oa meno manne,  kumtengua uti wa mgongo pamoja na kumsabishia ulemavu wa miguu.

Katika utetezi wake, mshtakiwa alidai alimpiga mwanawe huyo aliyekuwa akisoma darasa la tatu kwa sababu alikuwa hahudhurii masomo shuleni na badala yake alikuwa akiishia njiani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,673FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles