Muungano wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC),umeadhimisha kumbukumbu ya miaka minne ya kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi.
Katika maadhimisho hayo, Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji alilaani vitendo vya kuwapiga, kuwanyanyasa, kuwaharibia vifaa vya kazi na kuwaua waandishi wa habari kwa kuwa vinaminya uhuru wa habari nchini.
Naye Mkurugenzi wa UTPC, Aboubakar Karsan, aliwataka waandishi wa habari kujiunga na vilabu vya waandishi wa bahari nchini   viwasaidie   wanapopata matatizo wakiwa kazini.