27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Satelaiti ya Facebook Afrika yaharibiwa

Mark Zuckerberg
Mark Zuckerberg

FLORIDA, Marekani

MWANZILISHI wa Kampuni ya Facebook, Mark Zuckerberg, amesikitishwa na kitendo cha satelaiti ambayo Facebook ingeitumia kwa mawasiliano ya kasi ya mtandao wa intaneti barani Afrika kuharibiwa.

Satelaiti hiyo iliharibiwa katika mlipuko uliotokea Septemba mosi, mwaka huu eneo la Cape Canaveral jimbo la Florida, Marekani.

Satelaiti hiyo kwa jina la Amos-Six ilikuwa imebebwa na roketi ya Falcon Nine ambayo ililipuka ilipokuwa ikifanyiwa majaribio ya kujiandaa kwa safari.

Mlipuko huo ulitokea wakati roketi hiyo ikijazwa mafuta na kutikisa majengo yaliyokuwa umbali wa kilomita kadhaa.

Zuckerberg, ambaye yumo ziarani Afrika, alisema: “Nimesikitishwa sana kusikia kwamba satelaiti hiyo iliharibiwa. Tutaendelea kujitolea katika lengo la kufikisha huduma ya mtandao kwa kila mtu na tutatia bidii hadi kila mtu apate nafasi na manufaa ambayo yangetokana na satelaiti hii,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa kulipuka kwa roketi hiyo ni pigo kubwa kwa mwanabiashara, Elon Musk, ambaye ni mmiliki wa kampuni ya kuunda roketi ya Space X.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles