MAREKANI,
MKE wa mgombea urais nchini Marekani kupitia Chama cha Republican, Melania Trump, amelishtaki gazeti la Daily Mail la nchini Uingereza pamoja na mwanablogu wa Marekani akitaka alipwe dola milioni 150 sawa na Sh bilioni 300 kutokana na kumtuhumu kwamba alikuwa kahaba kati ya miaka ya 1990.
Gazeti hilo lililodokeza hilo ni Daily Mail ambalo lilidai kwamba huenda Melania alifanya kazi ya muda kama kahaba mjini New York na kwamba alikutana na mumewe Trump mapema kuliko inavyodaiwa.
Mwanablogu Webster Tarpley aliandika kwamba, Melania anahofia sana maisha yake ya awali yasifichuliwe kwa umma.
Wakili wa Melania, Charles Harder, alisema madai hayo ni ya uongo.
“Washtakiwa walitoa tuhuma kadhaa kuhusu Melania ambazo ni za uongo asilimia 100 na kumharibia sifa,” alisema Harder.
Gazeti la Daily Mail lilinukuu madai yaliyokuwa yamechapishwa na jarida moja la Slovenia kwa jina la Suzy kwamba wakala wa uanamitindo ambaye Melania alikuwa akifanyia kazi wakati huo pia alihudumu kama wakala wa kutafutia kazi makahaba na kwamba nyaraka za mahakama zinaonesha.