25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Neymar aipeleka Brazil fainali Olimpiki

Neymar de Santos
Neymar de Santos

RIO DE JANEIRO, BRAZIL

NAHODHA wa timu ya taifa ya Brazil kwa upande wa wanaume, Neymar de Santos, amefanikiwa kuipeleka timu hiyo katika hatua ya fainali kwenye michuano ya Olimpiki baada ya kuifunga Honduras mabao 6-0.

Huu ni ushindi wa pili wa nguvu kwa Brazil ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, awali walianza vibaya katika mchezo wa kwanza ambapo walilazimishwa suhulu dhidi ya Afrika Kusini, kabla ya kutoka suluhu nyingine dhidi ya Iraq.

Brazil ilianza kuinuka katika mchezo wao muhimu dhidi ya Denmark, ambapo mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa Brazil na kama wangepoteza basi wangeondolewa kabisa kwenye michuano hiyo, lakini walifanikiwa kuonesha uwezo wao na kushinda mabao 4-0.

Hata hivyo, walifanya vizuri kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Colombia, ambapo wenyeji hao walishinda mabao 2-0 na kuingia nusu fainali na kuwatembezea kichapo Honduras kwa mabao 6-0.

Nahodha wa timu hiyo ambaye anakipiga katika klabu ya Barcelona, Neymar, aliifungia timu hiyo mabao mawili na kuipeleka fainali, huku mabao mengine yakifungwa na Gabriel Jesus, ambaye alifunga mawili dakika ya 26 na 35, huku Marquinhos Correa akifunga bao dakika ya 51 na Luan Vieira dakika ya 79.

Mashabiki wa timu hiyo wameanza kuungana pamoja kuiunga mkono timu hiyo waliyokuwa wanaizomea katika michezo miwili ya awali, lakini kwa sasa wanaonekana uwanjani wakiwa na furaha kubwa na kuipa sapoti.

Neymar, ambaye ni mshambuliaji wa timu hiyo, amewataka mashabiki kuendelea kuiunga mkono timu hasa katika mchezo wa mwisho wa fainali ambao utapigwa kesho dhidi ya wapinzani wao Ujerumani.

“Tumepambana hadi kufikia hapa, bado tunaamini tuna nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa mwisho na kutwaa ubingwa wa michuano hii kwa upande wa soka.

“Najua mashabiki walikuwa hawana imani na sisi katika michuano hii hasa kutokana na kuanza vibaya katika michezo miwili ya awali, lakini kwa sasa tupo katika ubora wetu kwa ajili ya kuwania medali hiyo ya dhahabu,” alisema Neymar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles