30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kapombe kurudia kiwango chake

Shomari Kapombe
Shomari Kapombe

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

BEKI wa kulia wa timu ya Azam FC, Shomari Kapombe, amesema atahakikisha anafanya mazoezi zaidi na kurudi kwenye kiwango chake cha awali ili kuweza kupambana vema katika msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kapombe alikaa nje ya dimba kwa takribani miezi mitatu na kushindwa kumaliza vizuri msimu baada ya kuugua ugonjwa wa Pulmonary Embolism (donge la damu kuziba mishipa ya damu katika mapafu).

Akizungumza Dar es Salaam juzi baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ambao ulimalizika kwa jumla ya mikwaju ya penalti 4-1, Kapombe alisema anataka kuiletea ushindani timu yake na kufanikiwa kutwaa ubingwa katika ligi hiyo.

“Nimerudi baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kucheza, hivyo nawaomba mashabiki waendelee kutupa sapoti ili watuongezee morali na kufanya vizuri katika msimu mpya,” alisema.

Akizungumzia mchezo huo, Kapombe alisema baada ya kuwasoma wapinzani wao katika kipindi cha kwanza walifanikiwa kupambana na hatimaye  kusawazisha mabao yote yaliyopelekea kutwaa kombe hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles