26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Riyad Mahrez amalizana na Leicester City

Riyad Mahrez
Riyad Mahrez

LONDON, ENGLAND

NYOTA wa mabingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, Riyad Mahrez, amekata mzizi wa fitina na kuamua kumalizana na klabu hiyo kwa kusaini mkataba wa miaka minne.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alikuwa anahusishwa na kujiunga na klabu ya Arsenal, lakini hadi sasa dili hilo linaonekana kufikia mwisho baada ya kumalizana na klabu hiyo ya King Power.

Mkataba huo mpya utamfanya mchezaji huyo aendelee kuwa katika uwanja wa King Power hadi Juni 2020, huku akipokea kitita cha pauni 100,000 kwa wiki.

Hata hivyo, mchezaji mwenzake wa klabu hiyo, Jamie Vardy, ameonekana kufurahishwa na kitendo cha mpambanaji mwenzake kujitia kitanzi ndani ya klabu hiyo.

Kwa upande mwingine kocha wa klabu hiyo, Claudio Ranieri, amezidi kupata nguvu baada ya kumalizana na mchezaji huyo huku akiwa tayari amemkosa mchezaji wake muhimu katika safu ya kiungo, N’Golo Kante, aliyejiunga na klabu ya Chelsea.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, alionesha uwezo wa hali ya juu katika michuano ya Kombe la Euro 2016 nchini Ufaransa, akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, hivyo kuwashawishi Chelsea kuweka kitita mezani cha pauni milioni 32 katika kipindi hiki cha usajili.

Mwenyekiti wa klabu ya Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha, amefanya mazungumzo ya kina na Mahrez na kumwambia kwamba klabu hiyo inataka kuwapigania wale wote ambao walipambana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita, ili waweze kuendelea kukaa kwenye klabu hiyo kwa muda mrefu.

Hata hivyo, mshambuliaji mwingine wa timu hiyo, Jeffrey Schlupp, ambaye alikuwa anawindwa na klabu ya West Brom, amekubali kubaki kwa mabingwa hao na yupo tayari kwa dili jipya.

Mahrez, raia kutoka nchini Nigeria, alikuwa mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita, aliyefunga mabao 17 na kutoa pasi za mwisho 11. Alijiunga na klabu hiyo mwaka 2014, akitokea Le Havre ya nchini Ufaransa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles