25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Omog awafungia kazi washambuliaji Simba

1

Na THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM,

KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog, ameeleza anataka kuwa na washambuliaji wenye njaa ya mabao katika kikosi chake, hali inayomfanya kuwapigisha jaramba washambuliaji hao atakaowatumia kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, inayotarajia kuanza kesho ili kurudisha heshima ya timu hiyo kongwe nchini.

Omog ambaye ni Mcameroon anayelijua soka la Tanzania, ameona klabu nyingi za Tanzania zinakosa washambuliaji wenye uchu, hivyo kuamua kuwafungia kazi washambuliaji wake.

Katika mazoezi yake, Omog amekuwa akianza kuwanoa mastraika kwa saa moja, kabla ya kujumuika na wachezaji wenzao kwenye mazoezi ya saa kumi jioni.

“Ninaona washambuliaji wana kazi kubwa ndio maana nimeamua niwe nawanoa kwa muda wa peke yao, nawafundisha jinsi ya kufunga pia kupiga penalti, nataka wawe na uchu wa magoli na watumie nafasi kila wanapopata, hili litatusaidia sana,” alisema Omog.

Mazoezi ya jana yalihudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, ikiongozwa na Rais Evans Aveva, Collins Frisch, Said Tully na Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara.

Wakati huo huo, klabu ya Simba leo itafanya kisomo (khitma) na dua kwa ajili ya kuwarehemu wazee na waasisi wake waliotangulia mbele ya haki, likiwa ni zoezi la kila msimu kabla ya kuanza kwa ligi.

Manara alieleza shughuli hiyo itafanyikia katika Uwanja wa Bunju, ambao kwa sasa ujenzi wa awamu ya kwanza unaendelea.

“Dhumuni letu ni kumwomba Mwenyezi Mungu awarehemu wazee na waasisi wetu na pia kuiombea timu yetu, ifanye vzuri kwenye ligi pamoja na kutuepushia mabalaa ya ndani na nje ya uwanja kwa timu na klabu kwa ujumla,” alisema.

Alisema kisomo kitaanza saa saba mchana (baada ya swala ya Ijumaa) na kuhudhuriwa na baadhi ya wanachama watakaowawakilisha wengine, viongozi wa zamani wa klabu, wazee, waasisi na viongozi wa Serikali, wabunge, viongozi wa vyama vya siasa ambao ni wadau wa Simba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles