30 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Kenyatta, Raila wakubaliana kudhibiti wanaohama vyama

Uhuru Kenyatta
Uhuru Kenyatta

NAIROBI, KENYA

RAIS Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani wa Muungano wa Cord, Raila Odinga, wamekubaliana kuwazuia wagombea wa nafasi mbalimbali wanaohama vyama kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Pendekezo hilo linatarajia kujadiliwa katika Bunge la Taifa na Baraza la Seneti, liliungwa mkono na mungano ya Jubilee na Cord, ambayo ina wawakilishi wengi katika vyombo hivyo viwili vya maamuzi.

Kiongozi wa walio wengi bungeni, Aden Duale na mwenzake wa walio wachache, Francis Nyenze waliunga mkono muswada huo kupitia Tume ya Teule ya Pamoja ya Kibunge.

Mpango huo unalenga kukomesha vitendo vya wagombea wanaoteuliwa kuwania nafasi mbalimbali kuhamia vingine kwa lengo la hujuma.

“Hatupingi uamuzi wowote unaozuia kuhama vyama wakati wakihitajika lakini haimaanishi kuna ulazima wa kupitisha sheria, ni sisi tulioathirika huko nyuma na Jubilee waliokuwa wanufaika wa hujuma hizi baada ya wao kuwakuta, wameamua kuja na sheria hii, huu ni unafiki,” alisema Odinga.

Akizungumza na wanahabari juzi, Raila alisema wakati akikubali pendekezo hilo, anapinga kumhusisha Rais kupitisha makamishina wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)

Rais Kenyatta alitarajia kupokea ripoti ya IEBC jana.

Duale alisema ripoti na muswada ulioandaliwa na Kamati Teule ya Pamoja ya Kibunge, zitapitishwa kama zilivyo, akiongeza kuwa kipengele kinachozuia kuvitosa vyama kitapunguza kuibuka kama uyoga kwa vyama vidogo alivyoviita vya mfukoni wakati uchaguzi unapokaribia.

“Nchi hii inapaswa kuwa na vyama vitatu au vinne. Ni jambo jema kwa demokrasia,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles