25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Usain Bolt atetea ubingwa wake Olimpiki

Usain Bolt
Usain Bolt

RIO DE JANEIRO, BRAZIL

MWANARIADHA wa nchini Jamaica, Usain Bolt, amefanikiwa kutetea ubingwa wake kwa kutwaa medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki katika mbio za mita 100.

Bingwa huyo ameweka rekodi mpya ya kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda medali ya dhahabu kwa mara ya tatu mfululizo, katika mbio hizo za mita 100.

Bolt mwenye umri wa miaka 29, katika mbio hizo alitumia muda wa sekunde 9.81 katika fainali hiyo, lakini ameshindwa kufikia rekodi yake ambayo aliiweka mwaka 2009 jijini Berlin nchini Ujerumani, kwenye michuano ya dunia ya Championships, ambapo alitumia sekunde 9.58.

Katika hatua hiyo, Bolt alikutana na ushindani mkubwa na Justin Gatlin ambaye alitumia sekunde sawa lakini aliachwa kwa pointi 0.08 na kumfanya ashike nafasi ya pili na kuchukua medali ya fedha.

Hata hivyo, mpinzani huyo aliwahi kupigwa marufuku mara mbili kwenye riadha kwa matumizi ya dawa ambazo haziruhusiwi katika michezo.

Nyota huyo alikuwa na wakati mgumu baada ya kutajwa jina lake katika orodha ya watu ambao watashiriki michuano hiyo, mashabiki wengi walisikika wakimzomea mwanamichezo huyo raia wa nchini Marekani.

Kuzomewa huko kulitokana na tuhuma za kutumia dawa za kusisimua misuli, lakini hata hivyo alifanikiwa kuonesha uwezo wake na kushika nafasi hiyo ya pili.

Katika mbio hizo, nafasi ya tatu ilishikwa na mwanariadha raia wa nchini Canada, Andre de Grasse, ambaye alishinda medali ya shaba, baada ya kutumia muda wa sekunde 9.91.

Bolt baada ya kushinda medali hiyo, alikuwa na furaha kubwa na kudai kwamba alitarajia kuwa na kasi zaidi lakini hajafanya hivyo.

“Nilitarajia kuwa na kasi kubwa zaidi ya hii ambayo nimeionesha, lakini kikubwa ambacho ninakifurahia ni kwamba nimefanikiwa kuchukua medali hiyo ya fedha.

“Siku zote ushindani unakuwa mkubwa hasa katika michuano mikubwa kama hii ya kimataifa, nina furaha kwa kuwa ninawakilisha vizuri taifa,” alisema Bolt.

Bolt anatazamia kuondoka Rio na medali zaidi za dhahabu katika mbio za mita 200 na mita 100 kwenye mbio za kupokezana vijiti, kama ilivyokuwa kwenye michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 na 2012.

Mwanariadha huyo anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100, alisema atastaafu kutoka kwenye ulingo wa riadha baada ya michuano ya ubingwa duniani ya mwaka 2017.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles