27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wenger: Hatukuwa tayari kuwakabili Liverpool

11251590_arsenal-vs-liverpool-arsene-wengers-key_fb46baed_m

LONDON, ENGLAND

BAADA ya Arsenal kuchezea kichapo cha mabao 4-3 dhidi ya Liverpool, kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger, ameweka wazi kuwa timu yake haikuwa tayari kupambana na wapinzani hao.

Hata hivyo, kauli ya kocha huyo inaonekana kuwashangaza mashabiki wengi ikiwa ni siku saba tangu aweke wazi kwamba kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mikiki mikiki ya msimu mpya wa ligi.

Kocha huyo aliyasema hayo mara baada ya kushinda katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Manchester City.

“Tulikuwa hatupo tayari kimchezo dhidi ya Liverpool kwa kuwa kuna baadhi ya wachezaji ambao bado walikuwa hawajaungana na timu kutokana na kupumzika baada ya michuano ya Euro 2016.

“Hata kwa wale ambao wameungana na timu bado hawajaanza kuwa vizuri kama ilivyo kwa wenzao, lakini ninaamini baada ya muda kila kitu kitakuwa sawa na tutafanya vizuri.

“Kuna wachezaji ambao niliwakosa kwenye kikosi changu kutokana na sababu mbalimbali kama vile Mesut Ozil, Olivier Giroud, Laurent Koscielny, lakini hadi kufikia wiki ijayo watakuwa sawa.

“Lini tutakuwa tayari? Hata sijui ni lini lakini ninaamini wiki ijayo tutakuwa tayari kwa kuwa tunatakiwa kupambana na mabingwa watetezi, Leicester City kwenye uwanja wa ugenini,” alisema Wenger.

Kwa upande wake kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amedai kwamba alikuwa hana sababu ya kufurahia mabao dhidi ya wapinzani wake.

“Nimefanya makosa kushangilia ushindi kwa kuwa najua bado kuna safari na michezo mingine mbele. Arsenal ni timu kubwa katika ligi nchini England, huu ni mwanzo ninaamini watakuwa vizuri katika michezo ijayo,” alisema Klopp.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles