WANANCHI wa Kitongoji cha Isele Mamlaka ya Mji mdogo wa Ilula wilayani Kilolo, wamemwomba Rais Dk. John Magufuli kumtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji kwenda katika eneo lao ili kuweza kumaliza kero ya maji inayowakabili.
Wamesema kitendo hicho kimekuwa kikisababisha ndoa nyingi kuvunjika kwa sababu wanawake hulazimika kuamka usiku wa manane kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma ya maji.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake katika mkutano wa kijiji, Imelda Chonya, alisema kuwa hivi sasa wanalazimika kutembea kilometa tisa kwa ajili ya kutafuta maji katika jijini vya jirani na kushindwa kufanya shughuli nyingine za uzalishaji mali ikiwemo kilimo.
“Tatizo hili hapa kwetu Isele ni kubwa sana hasa kwetu sisi wanawake ambao tumeolewa kwani maji mara nyingi tunayapata usiku wa mananemaran yingi hutoka usiku wa manane au unafata kule vijiji vya jirani hili kwetu ni mateso makubwa.
“kwa hali hiyo tunamuomba Rais Magufuli au Waziri wa Maji aje hapa kwetu waone adha hii, kila mwaka sisi Isele tumekuwa tukipewa matumaini yasiyoonekana hili kwetu ni mateso na limetuchosha na sasa tunataka maji,” alisema Imelda.
Naye Latifa Kunzugula, alimuomba Rais Magufuli kuteleleza ahadi yake kwa vitendo ahadi aliyoitoa wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana kuwa atahakikisha Ikula maji yanafika wakati.
“Tunaamini Magufuli anasikia kilio chetu sisi tunamtaka yeye maana alisema madawati shule na elimu bure watendaji wote wametekeleza kwa nini maji tukose na tendo zetu sasa zipo hatarini jamani, Magufuli Rais wangu sikilia kilio chetu sisi,” alisema Latifa
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa hivi sasa watoto wao hulazimika kwenda shule asubihi kila kuoga hali inayosababisha kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ilula, Fransis Raymond (Chadema), alisema kuwa suala la maji katika mji wa Ilula limekuwa likitumika kama mtaji wa kisiasa lakini bado wananchi wanaendelea kuumia.
“Mimi ni mwanachi na adha wanayopata wenzangu nami inanikuta lakini masikitiko yangu ni kwa nini suala la maji limekuwa likitumiwa kama mtaji wa kisiasa. Kila mara nimejenga hoja katika vikao vya Baraza la Madiwani wanaandika utekelezaji hakuna sasa labda tumuombe Rais Magufuli atoa tamko maana alisema yeye ni rais wa Watanzania wote,” alisema