32.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya NMB yageukia sekta ya kilimo

nmbNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

BENKI ya NMB imezindua mpango mkakati wenye thamani ya Sh bilioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma zake za fedha kwa miaka mitano kwenye upande wa kilimo.

Mpango mkakati huo unahusu kupanua huduma za fedha kwenye mazao zaidi ya kilimo kutoka matano ya sasa hadi 12.

Kutokana na hali hiyo, benki hiyo imesema kuwa mpango huu utatoa fursa ya huduma za fedha sio tu kwa wakulima kupitia mfumo wa vikundi na kwa mkulima mmoja mmoja jambo ambalo litaongeza uzalishaji zaidi kupitia mnyororo mzima wa thamani katika kilimo.

Akizungumza katika uzinduzi huo juzi jijini Dar es Salaam,  Ofisa Mtendaji NMB, Ineke Bussemaker, alisema benki yake inatambua umuhimu wa sekta ya kilimo kwenye uchumi wa nchi.,

Kutokana na hali hiyo, alisema ndiyo maana imechukua juhudi za makusudi kuboresha na kupanua huduma za fedha zinazolenga kuikuza sekta ya kilimo.

“Kwa kuzingatia umuhimu wa kuboresha sekta ya kilimo Tanzania, tunalenga kujenga mazingira na taratibu ambazo mkulima mdogo na washiriki wote kwenye mnyororo huu wa thamani wataweza kuboresha ufanisi katika upatikanaji wa pembejeo, uzalishaji kwa njia za kisasa mbegu bora, mbolea, kutumia zana na nyezo mbalimbali za kilimo pamoja na ufanisi kwenye masoko. Yote haya yanawezekana kupitia upatikanaji wa uhakika wa huduma za fedha kwenye kilimo.

“NMB tunaona fursa kubwa sana kwenye sekta ya kilimo. Tunaamini kwa kuongeza ushiriki wetu kwenye sekta hii, kutakuwa na msukumo chanya kwenye maisha ya wakulima wetu na wote kwenye mnyororo wa thamani wa sekta hii, na vilevile kutimiza malengo ya NMB,” alisema Bussemaker.

Ofisa Mtendaji Mkuu huyo alisema kwamba tayari benki ya NMBT inawafikia wakulima wadogo wasiopungua 600,000 nchi nzima kupitia mpango mkakakati huo.

“Benki hii sasa inawalenga wakulima wakubwa, wafanyabiashara wa pembejeo, wachakataji wa mazao ya kilimo, wafanyabiasha wauzaji wa mazao na wahusika wengine wote kwenye mnyororo mzima wa thamani katika kilimo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles