25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mo Farah: Nipo tayari kwa michuano ya Olimpiki

 Mo Farah
Mo Farah

LONDON, ENGLAND

MWANARIADHA nchini England, Mo Farah, baada ya kushinda katika michuano ya Anniversary Games nchini humo, amedai kwamba kwa sasa yupo katika ubora wake na tayari kwa michuano ya Olimpiki.

Bingwa huyo katika michuano ya Anniversary Games, alifanikiwa kushinda kwa kukimbia umbali wa mita 5,000, hivyo amedai hana wasiwasi na wapinzani wake katika michuano ya Olimpiki ambayo itaanza Agosti 5 mwaka huu.

“Wakati nashiriki michuano hii ya Anniversary Games nilijiona kuwa sipo katika ubora wangu kutokana na maandalizi ambayo niliyafanya, lakini mwisho wa siku nimefanikiwa kushinda.

“Hii ni dalili tosha kwamba ninaweza kufanya vizuri zaidi katika michuano ya Olimpiki ambayo itaanza mwezi ujao.

“Najua kuna washindani wangu ambao wana uwezo mkubwa, ila sina wasi wasi, ninaamini nina uwezo wa kushinda kama nilivyoshinda huku.

“Najua nina wakati mgumu wa kutetea ubingwa wangu wa Olimpiki kutokana na wapinzani kutumia muda mrefu kujiandaa na michuano hii, lakini chochote kinaweza kutokea.

“Najua kuna wapinzani wangu watatu kutoka nchini Ethiopia, watatu kutoka Kenya na watatu kutoka nchini Uganda, hao wote wamejipanga kwa ajili ya kushindana na mimi.

“Lakini ninaamini nitafanya kile ambacho nimekifanya kwenye michuano hii ya Anniversary Games na kuendelea kufurahia mataji hayo yote mawili,” alisema Mo Faraha

Farah, mwenye umri wa miaka 33, anataka kuweka rekodi mpya ambayo iliwekwa mwaka 1976 na nyota wa mchezo huo, Lasse Viren, hivyo akiweza kutwaa ubingwa huo msimu huu atakuwa mtu wa pili kushinda ubingwa huo mara mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles