24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Guardiola: Nitashikana mkono na Mourinho

Real Madrid's Portuguese coach Jose Mour

BEIJING, CHINA

KOCHA mpya wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, amedai kuwa atasalimiana kwa kushikana mkono na mpinzani wake, Jose Mourinho, kwenye mchezo wao wa leo.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo kwenye uwanja wa Bird’s Nest, jijini Beijing, katika michuano ya Kombe la ICC, hivyo Manchester United watapambana na wapinzani wake, Manchester City.

Makocha hao walikuwa na upinzani mkubwa wakati wote wanazifundisha klabu kubwa nchini Hispania, hivyo wawili hao walikuwa hawana uhusiano mzuri na leo hii wanakutaka kwa mara ya kwanza tangu wajiunge na klabu za nchini England.

Hata hivyo, kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, ameweka wazi kwamba, japokuwa wamekuwa hawana ukaribu, lakini atahakikisha anasalimiana na kocha huyo kwa kushikana mkono.

“Bila shaka sisi ni makocha wapole, kwa nini asinishike mkono wakati wa kusalimiana? Hakuna sababu ambayo itamfanya asinisalimie au kunishika mkono, lakini katika mchezo huo kila mmoja anataka kushinda, mimi nataka kushinda na yeye anataka kushinda.

“Lakini tutakuwa hatupo kwenye Ligi, huu utakuwa ni mchezo wa kirafiki, hivyo chochote kinaweza kutokea kwa kuwa ni sehemu ya mazoezi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu nchini England,” alisema Guardiola.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba uwanja ambao watautumia leo ulinyeshewa na mvua kali wiki iliopita, hivyo haupo katika hali mzuri, Guardiola ana wasiwasi na wachezaji wake kupata majeraha kutokana na hali hiyo.

“Kuna taarifa nilizipata kwamba uwanja ambao tunataka kuutumia ulinyeshewa na mvua kali wiki iliyopita, sasa sijui upo katika hali gani, kama ni hivyo basi nina wasi wasi na wachezaji wangu kupata majeraha kwa kuwa uwanja haupo katika hali mzuri.

“Hata hivyo, ninaamini tutaweza kuzoea mazingira, tutahakikisha tunafanya vizuri na kushinda kama tulivyopanga, lakini jambo muhimu ambalo tunataka kuliangalia ni wachezaji wangu wasipate majeraha,” aliongeza.

Kocha huyo ameweka wazi kwamba nahodha wake, Vincent Kompany, amerudi katika nafasi yake baada ya kuwa majeruhi kwa muda. Mchezaji huyo alikuwa nje ya uwanja katika mchezo wa kwanza dhidi ya Bayern Munich, huku Guardiola akipokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya timu yake hiyo ya zamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles