CALIFORNIA, MAREKANI
Mume mtarajiwa wa Blac Chyna ambaye ni kaka wa Kim Kardashian, Rob Kardashian ameshtakiwa kwa kuendesha gari kwa kasi huku akiwa na mpenzi wake mwanzoni mwa mwaka huu.
Rob mwenye umri wa miaka 29, alifikishwa mahakamani, kwa kosa hilo na kutakiwa kulipa faini ya dola 1,100 na kufungiwa kuendesha gari hadi pale atakapo ruhusiwa.
Inadaiwa kwamba hiyo sio mara ya kwanza kwa Rob kukamatwa kutokana na kosa kama hilo, awali aliwahi kukamatwa kwa kosa la kutumia leseni ambayo muda wa matumizi umekwisha.
“Ni kweli nimefanya kosa na natakiwa kuwajibika, haya ni makosa ya kawaida japokuwa mwendo kasi unahatarisha maisha yangu, hivyo nastahili kuwajibika,” alisema Rob