26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Taylor aongozwa kwa kulipwa duniani

Taylor Swift
Taylor Swift

NEW YORK, MAREKANI

Nyota wa muziki nchini Marekani mwenye umri wa miaka 26, Taylor Swift, ametajwa kuwa ni msanii ambaye anaongoza kwa kulipwa fedha nyingi kwa sasa.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes, msanii huyo anadaiwa kuwa na kiasi cha dola milioni 170, huku akiwa kati ya mastaa 100 wenye fedha nyingi.

Wakati huo Jay Z na mke wake Beyonce kwa ujumla wanadaiwa kuongoza huku wakiwa na kiasi cha dola milioni 170.5, wasanii wengine ambao wametajwa na jarida hilo ni pamoja na Adele, ambaye anashika nafasi ya 9 akiwa na dola milioni 80.5.

Wakali wengine ni pamoja na Madonna ambaye anashika nafasi ya 12, akiwa na kitita cha dola milioni 76.5, Rihanna akishika nafasio ya 13 akiwa na kiasi cha dola milioni 75 na Katy Perry akishika nafasi ya 63 akiwa na dola milioni 41.

Mpenzi wa zamani wa Taylor, Calvin Harris ambaye ni nyota wa filamu nchini humo, anashika nafasi ya 21, akiwa na dola milioni 63.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles