27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Afrika Kusini yatawala vyuo vikuu bora Afrika 2016

Wanafunzi wa chuo kikuu nchini Afrika Kusini.
Wanafunzi wa chuo kikuu nchini Afrika Kusini.

Na JOSEPH HIZA – MASHIRIKA YA HABARI

SAFARI hii tunawaletea ligi ya vyuo vikuu Afrika, ambavyo kwa kawaida huwa havionekani katika orodha ya juu ya vyuo vikuu duniani, vikishindwa hata kuwamo walau katika 100 au 200 bora ijapokuwa mara kadhaa Afrika Kusini imekuwa ikiingia katika 200 bora.

Sababu kuu ya kukosekana kwa vyuo vikuu vya Afrika katika orodha za juu za ligi mbalimbali duniani ni aina ya vigezo vinavyotumika katika upimaji wa ubora wa taasisi hizo za elimu kutokuwa rafiki kwa Afrika.

Hiyo ni pamoja na suala la ubora wa miundombinu, ukosefu wa fedha za kutosha kwa shughuli mbalimbali za uendeshaji hasa tafiti pamoja na ubora wa taaluma yenyewe unaochagizwa na sababu kama vile mazingira mabaya ya kujisomea au kazi, maslahi duni kwa wahadhiri na kadhalika.

Tukirudi katika ligi ya vyuo vikuu Afrika kwa kutumia vigezo zinavyotumiwa na taasisi ya World University Rankings (WUR), katika 15 bora, Afrika Kusini imetoa vyuo sita ikiwamo vinara watatu: Chuo Kikuu cha Cape Town (UCT), Chuo Kikuu cha Witwatersrand na Chuo Kikuu cha Stellenbosch.

Michael Sanne, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Uhandisi Umeme na Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Cape Town, anasema: “alichagua UCT kwa sababu aliona ndiyo chuo kikuu kizuri na bora zaidi kuliko vyote alivyoviona Afrika Kusini.

“Kitaaluma nimekumbana na changamoto nyingi kuliko nilivyotarajia lakini nimejifunza mambo mengi mazuri na yenye umuhimu katika kila siku iendayo kwa Mungu.”

Vyuo vikuu nchini Uganda (Makerere), Ghana (Ghana), Kenya (Nairobi), Misri (Mfereji Suez, Alexandria na Cairo ), Morocco (Marrakech Cadi Ayyad na Mohammed V) na Nigeria (Ibadan) pia vilikuwa ndani ya 15 bora.

Chuo Kikuu cha Mohammed V of Rabat nchini Morocco kilifunga katika 15 bora na ni chuo kikuu pekee katika orodha ya Afrika ambacho hakikuweza kuingia katika orodha bora ya World University Rankings.

Kwa ujumla, vyuo vikuu katika orodha vina asilimia ndogo ya wanafunzi wa kimataifa katika kampasi wa kati ya asilima moja na tisa, isipokuwa UCT, kilichokuwa na asilimia 18 ya wanafunzi wa kimataifa.

Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda ambacho kilishika nafasi ya nne katika orodha hiyo kilikuwa na asilimia tisa ya wanafunzi wa kigeni katika kampasi zake.

Mwanafunzi wa shahada ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma chuoni hapo, Musinguzi Blanshe anasema: “Kijamii nilikutana na wanafunzi kutoka nje kama Kenya, Rwanda, Tanzania na maeneo mengine. Kuishi katika jamii yenye mseto wa utamaduni kumeimarisha ufahamu wangu na ninashukuru kwa mseto huu.”

Wakati Tanzania ikishindwa kutoka katika orodha hiyo ya WUR ikiwa imeitosa Tanzania kutoka 15 bora kutokana na kigezo cha wingi wa wanafunzi wa kimataifa imeweza kutoka katoka orodha ya 200 bora ya University Web Ranking ambayo inaangazia namna vyuo vikuu vilivyozitendea haki tovuti zao.

Katika 15 bora chuo kikuu cha Dar es Salaam kilishika nafasi ya 11 kikifuatiwa na Chuo Kikuu cha Nairobi. Katika ligi hii vyuo vikuu vya Afrika Kusini kama kawaida viliendelea kutamba ikitoa vyuo tisa huku Misri ikiendelea kushika nafasi ya pili kwa vyuo vinne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles