Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), kimetangaza kufanyika mkutano wake mkuu wa mwaka Julai 23, mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo, ilieleza kuwa mkutano huo utakuwa na ajenda sita ambazo zitajadiliwa na wanachama.
“Tunafanya mkutano mkuu wa mwaka kutimiza masharti na matakwa ya Katiba. Mkutano huu huwashirikisha wanachama wote ambao ni hai wa JET.
“… ndiyo maana nasisistiza hapa wenye haki ya kuhudhuria mkutano huu ni wale waliolipa ada kwa mujibu wa utaratibu. Ajenda zikazowasilishwa ni kufungua mkutano,
dondoo za mkutano wa mwaka uliopita, yatokanayo na mkutano mkuu uliopita.
“Nyingine ni ripoti utendaji, ripoti mkaguzi wa hesabu na bajeti 2015 na mengineyo,” alisema Chikomo
Mkiurugenzi huyo wa JET alisisitiza kuwa wenye haki kuhudhuria mkutano mkuu huo wa mwaka ni wale tu waliolipa ada zao hadi kufikia Desemba mwaka 2015.