32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi za dini zarudishiwa msamaha wa kodi

Philip MpangoNa Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI  wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema amefuta utaratibu alioupendekeza bungeni wa taasisi za dini kulazimika kulipa kodi kwanza kwa bidhaa watakazonunua au kuagiza kutokana nje ya chini.

Kutokana na utaratibu huo wa awali wa Serikali taasisi hizo za dini zilitakiwa kulipa kodi hiyo na kisha kurejeshwa baada ya ukaguzi kufanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, kuhusu ufafanuzi wa baadhi ya hoja za wabunge kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Alisema kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji huduma za elimu na afya anapendekeza kufuta utaratibu huo na badala yake Serikali itaimarisha zaidi hatua mbalimbali za udhibiti wa msamaha ya kodi.

Alisema uamuzi huo wa Serikali umetokana na maombi na mapendekezo mbalimbali ya wadau yaliyoitaka serikali iendelee kutoa misamaha ya kodi kwa taasisi hizo kutokana na umuhimu wake wa kuisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi hizo.

“Kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji; nimeamua kufuta utaratibu nilioutangaza katika hotuba ya bajeti, badala yake serikali itaimarisha zaidi udhibiti wa misamaha hiyo,” alisema Dk. Mpango

Alizitaja baadhi ya hatua zitakazochukuliwa kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo kuwa ni kuzitaka taasisi za dini kuwasilisha orodha ya vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwanzo wa mwaka wa kalenda, pamoja na kuthibitisha kama vifaa vilivyosamehewa kodi mwaka uliotangulia vilitumika kwa mujibu wa sheria

Kutokana na hali hiyo utaratibu mpya utazitaka taasisi hizo za dini kuwasilisha majina ya watu waliowaidhinisha kuandika barua za maombi ya msamaha wa kodi zikiainisha cheo, saini, picha, anuani na namba za simu za wahusika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles