25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Iran kununua ndege 100 kutoka Marekani

MAMLAKA ya Usafiri wa Ndege nchini IranTEHRAN, IRAN

MAMLAKA ya Usafiri wa Ndege nchini Iran zimetangaza kuwa itanunua ndege 100 kutoka kampuni ya uundaji ndege ya Boeing, nchini Marekani.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Iran, kwa sasa pande hizo mbili zinasubiri idhini kutoka Hazina ya Marekani.

Aidha Januari mwaka huu, Iran ilifikia makubaliano na Marekani kununua zaidi ya ndege 100 kutoka kampuni ya uundaji wa ndege barani Ulaya ya Airbus.

Makubaliano ya sasa yanathibitisha taarifa iliyotolewa Juni 6 mwaka huu na Shirika la Habari la Uingereza (Reuters) kuwa Iran ipo njiani kufikia makubaliano ya kihistoria ya kununua ndege kutoka kampuni ya Marekani.

Ununuzi huo kutoka Marekani utakuwa wa kwanza tangu mapinduzi ya Kiislamu ya taifa hilo mwaka 1979.

Idhini ya Marekani kwa Boeing kuanzisha mazungumzo ya kibiashara na Tehran Februari mwaka huu ilitokana na kuondolewa japo kwa kiasi kidogo kwa vikwazo vya kiuchumi, baada ya makubaliano ya kupunguza mpango wake wa nyuklia.

Iran inajikakamua kununua ndege mpya za kibiashara, kuchukua mahala pa ndege zake zilizozeeka ili kupanua sekta yake ya uchukuzi wa anga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles