29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Uchaguzi waipeleka Yanga Ulaya

yanga shangweZAINAB IDDY NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

UCHAGUZI Mkuu wa klabu ya Yanga unafanyika leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam huku timu hiyo ikitarajiwa kuondoka kesho kwenda Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mchezo wake na Mo Bejaia.

Mchezo huo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, unatarajiwa kuchezwa Juni 19 nchini Algeria.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Baraza la Michezo Taifa (BMT), kuwataka wafanye uchaguzi ndani ya mwezi huu baada ya kutofanya hivyo kwa miaka miwili tangu walipoingia madarakani.

TFF ilipanga uchaguzi wa Yanga ufanyike Juni 25 mwaka huu na ilianza kutoa fomu lakini siku chache baadaye tangu TFF itangaze zoezi la uchukuaji fomu, Yanga nao wakatangaza  kufanya uchaguzi Juni 11 mwaka huu.

Hata hivyo, Jumanne iliyopita TFF ilikutana na viongozi wa Yanga na kuweka mambo sawa na ndipo shirikisho hilo lilipoubariki uchaguzi huo utakaofanyika leo.

Katika uchaguzi huo nafasi zinazowaniwa ni  Mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji.

Miongoni mwa wanaowania nafasi hizo katika nafasi ya ujumbe ni Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi, Bakari Malima,  Godfrey Mheluka na Lameck Nyambaya.

Wengine ni David Ruhago, Sylvester  Haule, Pascal Laizer, Samwel Lukumay, George Manyama, Hussein Nyika, Beda Tindwa, Tobias Lingalangala, Athuman Kihamia, Mchafu Chokoma na Sizi Lyimo, ambaye ni mwanamke pekee.

Makamu mwenyekiti ni Tito Othoro na Clement Sanga huku aliyekuwa mwenyekiti  wa timu hiyo akitetea kiti chake.

Wakati huo huo, wapinzani hao wa Yanga, Mo Bejaia imemtangaza Nacer Sandzak kuwa kocha mpya.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, Rais wa klabu hiyo, Zahir Attia, amefanikiwa kupata saini ya kocha huyo hivi karibuni ambaye alikuwa kiungo wa zamani wa timu ya JSKabylie Kamel Yesli.

Kocha huyo ameahidi usajili mkubwa ndani ya klabu hiyo kabla ya mchezo dhidi ya Yanga.

Hata hivyo, tayari wachezaji wawili wa nafasi ya kiungo, Zidane Mebarakou na Mouhamed Ndoye, watakosa mchezo  dhidi ya Yanga kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

Mchezo huo unatarajia kuchezeshwa na mwamuzi kutoka Morocco, Bouchaib Al-Ahrach na kusaidiwa na Achik Reddouane na Youssef Mabrouk.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles