26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 14 mbaroni kwa tuhuma za unyang’anyi

Wilbrod-MutafungwaNa Upendo Mosha, Moshi

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashilia watu 14 wakiwemo waganga wa kienyeji na wapishi kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha katika matukio mbalimbali ya uporaji yaliyowahi kutokea mkoani hapa.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wilbroad Mutafungwa, alisema watu hao walikamatwa kwa nyakati tofauti na makachero wa Jeshi la Polisi baada ya uchunguzi mkali kufanyika.

“Katika jitihada za kukabiliana na uhalifu tumefanikiwa kuwakamata watu 14 kwa kujihusisha na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo kati yao 10 ni majambazi sugu.

“Wengine wawili waganga wa kienyeji ambao huwahifadhi na kuzindika silaha zao pamoja na wasichana wawili ambao walikuwa wakitumika kuwapikia chakula, kuuza mali za wizi na kubeba silaha za majambazi hao,” alisema.

Kamanda Mutafungwa alisema katika mahojiano na majambazi hao, waliwataja waganga hao wa kienyeji kuwa wanawapatia dawa ili wasiweze kukamatwa  ambapo waganga hao walifuatiliwa na kukamatwa katika Wilaya ya Lushoto  mkoani Tanga ambao ni Suphiani Juma (66) na Upendo Rajabu (72), wote wakiwa ni wakazi wa wilayani humo.

Aliwataja wasichana waliokuwa wakisaidia kutoa huduma kwa majambazi hao kuwa ni Daines Salmu (17) ambaye ni fundi cherehani na Happy Mlay (22) wote wakiwa ni wakazi wa Kisangesangeni wilayani Moshi Vijijini mkoani hapa.

Alisema polisi baada ya upekuzi walikamata mali mbalimbali za wizi ikiwemo gari aina ya Noah nyeupe yenye namba za usajili T 642 CNU, ambayo ilipopekuliwa ilikutwa na silaha mbalimbali za jadi, pikipiki tatu na kwamba walikuwa wakizitumia kufanikisha matukio ya ujambazi.

Pia walikutwa na  bastola  aina ya Brown  iliyoibiwa  Februari 25 mwaka huu kutoka kwa mwanajeshi mstaafu wa JWTZ, Elibariki Urio (67) mkazi wa Marangu Samanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles