28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yasisitiza matumizi bora nishati ya umeme kulinda mazingira

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Watanzania wametakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika matumizi bora ya nishati ya umeme ili kupunguza upotevu, gharama na kulinda mazingira.

Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 5,2024 na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, alipokuwa akizungumzia mkutano wa kikanda wa matumizi bora ya nishati kwa nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika hapa nchini mwezi ujao.

Amesema kiwango cha upotevu wa umeme kwa sasa kimefikia asilimia 14 kutoka kiwango cha awali cha asilimia 21 na mkakati ni kufikia asilimia 9 kiwango kinachostahili.

“Tumendaa mkakati wa miaka kumi (2024 – 2034) wa matumizi bora ya nishati na tayari tumeandaa viwango vya matumizi bora ya nishati ambapo Shirika la Viwango nchini (TBS) limeweka viwango kwenye vifaa mbalimbali kama vile majokofu, kompyuta, taa…tunawaomba wananchi watumie vifaa vyenye viwango,” amesema Mhandisi Luoga.

Naye Mtaalam wa Miradi kutoka Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), Abbas Kitogo, amesema mradi wa matumizi bora ya nishati ambao ulikuwa ukamilike mwezi ujao umeongezewa muda hadi Novemba mwakani pamoja na kuongeza ufadhili wa masomo kwa wasichana 10 katika ngazi ya Shahada ya Uzamili.

Mkutano wa kikanda wa matumizi bora ya nishati utafanyika Desemba 4 hadi 5 jijini Arusha na kukutanisha wadau wa nishati zaidi ya 400 wakiwemo mawaziri, viongozi wa sekta binafsi na wataalam mbalimbali kujadili fursa na changamoto katika matumizi bora ya nishati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles