26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 19, 2024

Contact us: [email protected]

CUF wataka orodha wapigakura serikali za mitaa ikaguliwe

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Chama cha Wananchi (CUF) kimependekeza orodha ya wapigakura waliojiandikisha kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikaguliwe kujiridhisha kama wamekidhi vigezo.

Uandikishaji wapigakura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulianza Oktoba 11,2024 na unatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 20,2024 huku uchaguzi huo ukitarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.

Akizungumza Oktoba 18,2024 na Waandishi wa habari Naibu Katibu Mkuu wa Cuf – Bara, Magdalena Sakaya, amesema ukaguzi huo utasaidia vyama kujiridhidha iwapo walioandikishwa wamekidhi sifa na vigezo vinavyotakiwa.

“Tunatoa wito kwa waziri kutoa tamko kwa wasimamizi, wasimamizi wasaidizi na waandikishaji kuondoa kasoro zote kwenye orodha ya wapigakura na kuhakikisha siku zilizobaki zinatumika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu…orodha ikaguliwe ili kujiridhisha waliotimiza sifa tu ndiyo watapiga kura,” amesema Sakaya.

Sakaya amesema wamebaini kuwapo kwa mapungufu katika zoezi la uandikishaji wapigakura na kuziomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua na kuingilia kati haraka ili kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu zinafuatwa katika mchakato huo.

Chama hicho kimesema kimeandaa watu wenye sifa, weledi na wanaojitambua kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo na kuhakikisha kwamba wanasimamia ipasavyo maendeleo ya watu na taifa kwa ujumla.

Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tamisemi, Mohamed Mchengerwa, aliwataka wasimamizi wa uchaguzi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni pamoja na maelekezo ya usimamizi wa uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles