25 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya Akiba yawatunuku tuzo wateja wake

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Benki ya Akiba (ACB) imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kutoa tuzo kuthamini mchango wa wateja wake katika utoaji huduma za kibenki.

Tuzo hizo zimetolewa Oktoba 9,2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba, Silvest Arumasi, katika hafla iliyofanyika katika tawi la Ubungo la benki hiyo.

Arumasi amewashukuru Watanzania kwa kuungana nao katika safari ya kutoa huduma bora zaidi za kibenki ambazo zinachangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

“Nawashukuru wateja wetu kwa kutuchagua kuwa washirika muhimu wa kibiashara, bila ninyi tusingeweza kufikia mafanikio tunayojivunia sasa. Wiki hii ni maalumu kwa ajili ya wateja wetu kwa kuwa tunathamini na kutambua mchango wao,” amesema Arumasi.

Benki hiyo imefanya maboresho mbalimbali kama vile huduma za kidijitali kwa kuboresha huduma za ACB Mobile na Akiba Wakala kwa kuzingatia mahitaji ya wateja.

Mkurugenzi huyo amesema pia huduma mpya ya Internet Banking inayopatikana kwa wateja binafsi, makampuni makubwa na taasisi mbalimbali ni sehemu ya mkakati wa mabadiliko ya kidijitali wa benki hiyo wenye kaulimbiu ‘Twende Kidijitali’.

“Mwaka 2024 tumeamua kuupa jina la Mwaka wa Kidijitali na tumejidhatiti kuwafikishia huduma za kibenki kwa njia ya kisasa zaidi kupitia mifumo yetu ya kidijitali,” amesema Arumasi.

Aidha amesema benki itaendelea kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa wateja ili kuboresha bidhaa na huduma zake.

“Wiki hii siyo tu kwa ajili ya sherehe, bali ni ahadi yetu ya kuendelea kuboresha na kutoa huduma bora ambazo zitazidi matarajio ya wateja wetu,” amesema.

Kuhusu Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu yaani ‘Above and Beyond’ ikimaanisha kwenda zaidi ya matarajio; amesema inalenga kuhamasisha utoaji wa huduma bora zaidi kwa wateja.

Benki ya Akiba inatumia maadhimisho ya mwaka huu kufanya shughuli mbalimbali katika matawi yake yaliyopo Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Mbeya na Dodoma ili kuwapa fursa wateja ya kuona maboresho yanayoendelea kufanywa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles