29.3 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa afya awahakikishia Ruvuma uboreshaji wa huduma za afya

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama amewahakikishia wanaruvuma kuwa Serikali kupitia wizara hiyo, itaendelea kuboresha huduma za afya ikiwemo upatikanji wa vifaa, vifaa tiba pamoja na dawa.

Waziri Mhagama amesema hayo leo Septemba 20, 2024 baada ya kuwasili mkoani Ruvuma na kupokelewa na Mkuu wa mkoa huo, Ahmed Abbas.

Amesema Mkoa huo utanufaika na ujenzi wa wodi maalum za watoto wachanga waliozaliwa na uzito pungufu (NCU) ili kufikia lengo la Serikali kupunguza vifo vya watoto.

Kuhusu suala la lishe, Waziri Mhagama amesema Serikali inaendelea na zoezi la kutoa elimu kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ambao katika kila kitongoji watakua wawili (Wakike na Wakiume) watakaotoa elimu na huduma za kijamii za awali kwa wananchi.

Ziara ya Waziri Mhagama mkoani Ruvuma inafanyika siku chache kabla ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan itakayoanza Septemba 23 mkoani humo.

Waziri Mhagama akiwa mkoani Ruvuma anatarajia kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Jimbo la Peramiho ikiwemo kukagua utoaji wa huduma kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma (RRH), kukagua utekelezaji wa mradi mpya (New OPD) pamoja na kuzungumza na Watumishi wa Sekta ya Afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles