26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Rais IPU aimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Falme za Kiarabu

Na Mwandishi Wetu

Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk. Tulia Ackson, amekuwa katika ziara mbalimbali za kukutana na viongozi wa mabunge duniani kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kushughulikia changamoto zinazoikabili dunia kwa pamoja.

Katika ziara yake ya hivi leo Septemba 17 2024, amekutana na Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Saqr Ghobash, katika Abu Dhabi.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Viongozi hao waligusia ushirikiano katika nyanja mbalimbali kama vile uchumi, jamii, na siasa, huku wakiangazia umuhimu wa kushirikiana ili kuleta ustawi wa wananchi wao.

Pia walitilia mkazo ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu, kwa lengo la kukuza mafanikio ya pamoja na kuhakikisha maendeleo endelevu.

Taasisi ya IPU inatetea haki na amani duniani kupitia ushirikiano wa mabunge ya nchi mbalimbali. Dk. Tulia Ackson, kama Rais wa IPU, ana jukumu la kuhakikisha nchi wanachama zinashirikiana katika kushughulikia changamoto za kiuchumi, kijamii, na kisiasa zinazoikumba dunia, ikiwa ni pamoja na kukuza demokrasia na utawala bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles