Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Jumla ya klabu 14 kutoka Tanzania, Kenya na Uganda zinashuana katika mashindano ya Wazi ya Taifa yanayoendelea kwenye Bwawa la kuogelea la Shuke ya Kimataifa Tanganyika (IST), Masaki, jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yanahusisha vijana mwenye umri kuanzia miaka 9-23, lengo likiwa nin kupunguza muda wao.
Akizungumzia mashindano hayo ya siku mbili yanayofikia tamati kesho, Mwenyekiti wa Chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania( TSA) David Mwasyoge , amesema mchezo huo kwa sasa unashika kasi na amefurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na waogeleaji wanaoshiriki.
“Shindano hili limekuwa na ubora mkubwa kutokana na ongezeko kubwa la waogeleaji tofauti na ukilinganisha na mashindano yaliyofanyika siku za nyuma, amesema Mwasyoge.
Amesema waogeleaji wanaoshindana hapo wale ambao wamekidhi vigezo vya ushiriki wa Kimataifa.