33.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia aipa Serengeti Girls milioni 30

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Million 30 kwa timu Taifa ya wasichana ‘Serengeti Girls’, baada ya kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa nchi za Kaskazini mwa Afrika (UNAF U-17) katika mashindano yaliyofanyika nchini Tunisia 2024.

Akikabidhi kitika hicho leo Septemba 11, 2024 jijini Dar es Salaa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amewapongeza wachezaji hao kwa kuiwakilisha vyema Taifa huku akiwataka kujituma na kupambana zaidi ili kujipatia nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa kwa ajili ya kujenga timu ya taifa imara ya wanawake.

“Rais Samia amefurahishwa sana na ushindi huo na kutoa zawadi ya mama kwa kutoa kiasi cha milioni 30, kwa kuwakabidhi milioni 10 na kesho kutwa (ijumaa, Agosti 12) tutawamalizia milioni 20 kwa sababu ya changamoto ya mfumo,” amesema Dk. Ndumbaro

Aidha, Ndumbaro ameongeza kuwa ni maelekezo ya Rais Samia kuwa, wahakikishe timu zote za Taifa zinafanikiwa kufuzu fainali za AFCON pamoja na Kombe la Dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles