25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Shughuli za Utalii hifadhi ya Ngorongoro zinaendelea

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imewatoa hofu watanzania kuwa shughuli za utalii katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro zinaendelea vizuri pamoja na uwepo wa baadhi ya wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo kuandamana tarehe 18.08.2024.

Hayo yamebainishwa na Kaimu meneja, kitengo cha uhusiano na umma, Hamis Dambaya kupitia taarifa kwa umma aliyoitoa kuhusu hifadhi ya ngorongoro na uwepo wa muingiliano wa shughuli mbalimbali za kibinadamu.

Aidha Dambaya amesema kuwa bado Watalii kutoka ndani na nje ya nchi wameendelea na safari zao za kushuhudia vivutio vya utalii ndani ya hifadhi na Serikali inaendelea na kuwatoa hofu kwa kuwahakikishia usalama wao katika sehemu mbalimbali za vivutio vya hifadhi hiyo.

Dambaya amesema maandamano yaliyoripotiwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii yanaidhihirishia dunia na jumuiya za kimataifa, vyombo vya habari na asasi za kimataifa kwamba ndani ya Hifadhi hiyo hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu na unyanyasaji wa wananchi.

Hata hivyo mamlaka inawahakikishia watalii wote waliopanga safari za kuja Ngorongoro kuwa Serikali itaendelea kusimamia usalama wao wakati wote watakapokuwa ndani ya hifadhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles