32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mikakati ya Rais Samia yapaisha kilimo cha tumbaku

N Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MAAMUZI yaliyochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, yameiwezesha sekta ya tumbaku nchini kukua na kufika namba mbili Afrika kwa uzalishaji wa sekta hiyo.

Wakati Rais Samia anachukua madarasa ya urais, Tanzania ilikuwa inazalisha tani 65,000 za tumbaku wakati leo nchi inazalisha tani 122,000 na kuiwezesha kushika namba mbili Afrika kwa uzalishaji nyuma ya Zimbabwe.

Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa Kiwanda cha Sigara cha Serengeti, kilichopo mkoani Morogoro, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan alisema tumbaku yote itakayozalishwa na wakulima mashambani itanunuliwa.

“Sasa wakulima wataondokana na ‘grade’ ya uuzaji wa tumbaku kiwandani, maana nchi yetu sasa haitabakiza tumbaku majumbani kama zamani na kukuza uchumi wa wakulima na nchi yetu,” alisema Dk. Samia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles