23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU Kagera yarejesha milioni 4.3 za TASAF

Na Renatha Kipaka, Kagera

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imerejesha kiasi cha shilingi milioni 4.3, fedha ambayo ilipaswa kulipwa kwa wanufaika 139 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Kumtama, Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera.

Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoani hapo, Ezekia Sinkala, alitoa taarifa hiyo jana wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu kwa mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu kwa vyombo vya habari mjini Bukoba.

Sinkala alisema kuwa fedha hizo zilichukuliwa na wasimamizi wa zoezi la uhaulishaji wa fedha za TASAF kwa kipindi cha mwezi Mei hadi Juni na Julai na Agosti, ikiwa ni mgao wa madirisha mawili.

Amesema, taarifa za ubadhirifu huo zilitolewa katika mkutano wa hadhara uliokuwa ukihitaji kutatua kero ya wananchi wanaonufaika na mpango huo.

“Baada ya kupata taarifa hizo, uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa kiasi cha shilingi milioni 9.3 kilitakiwa kupelekwa kwa malipo ya awamu zote mbili katika kijiji cha Kumtama,” alisema Sinkala. “Fedha ya awamu ya kwanza ilikuwa shilingi milioni 4.6, lakini kwa makusudi, wasimamizi walitumia uelewa mdogo wa wanufaika.”

Aidha, amesema kuwa baada ya mahojiano, wasimamizi hao, ambao ni watumishi wawili wa Halmashauri ya Ngara, mtendaji wa kata, mwenyekiti wa kitongoji, na mwenyekiti wa kijiji walikiri kuchukua fedha hizo na kuahidi kuzirudisha.

Ameongeza kuwa sehemu ya fedha hizo zilipelekwa kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo na kurejeshwa kwa wananchi wanufaika mnamo mwaka 2021, ingawa zoezi hilo lilifanyika Septemba 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles