32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mtendaji Mkuu BRELA awataka wananchi kutembelea banda lao Sabasaba

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa, amewaomba wananchi kutembelea banda lao ili kupata huduma zote zinazotolewa na ofisi yao, huku wakitoa pia elimu kwa umma.

Akizungumza Julai 3, 2024, baada ya ufunguzi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (DIT) na kupokea tuzo kutoka kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya mshindi wa tatu kwa ujumla, Nyaisa alisema ushindi huo umetokana na utendaji kazi wao bora.

“Tunapoelekea, tunataka kuona kile tulichofanikiwa kukipata leo ndani ya maonesho haya kikiwa kama njia katika utendaji wetu wa kazi,” alisema Nyaisa.

Amesema uwepo wa tuzo hiyo inawakumbusha walipotoka, walipo, na wanapotakiwa kwenda katika kutoa huduma kwa wananchi.

Ameongeza kuwa katika maonesho ya mwaka huu hawakuja kuonesha tu huduma zao bali wamekuja kufanyakazi, kwani watendaji wote wametoka ofisini na kuja kwenye viwanja hivyo kuwahudumia wananchi.

“Nitoe rai kwa wananchi wote kuja kupata huduma hapa hapa kwenye maonesho. Utaweza kusajili kampuni, majina ya biashara, na vitu vingine na utakabidhiwa cheti chako hapa hapa. Sasa hatujaja kuonesha tu tunachokifanya bali tumekuja kukifanya kabisa hapa hapa,” alisema Nyaisa.

Aidha, alisema kwa sasa wanafanya kazi kidigitali katika kutoa huduma na wafanyakazi wamekuwa na morali ya kufanya kazi ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles