23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Makamu wa Rais mgeni rasmi kongamano Dira ya Maendeleo

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa kongamano la Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 litakalofanyika Juni 8,2024 kwenye ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 4, 2024 jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru amesema kongamano hilo linalenga la kukusanya maoni na kutoa elimu kuhusu Tanzania tuitakayo ifikapo 2050.

Amesema kuwa ushiriki wa utoaji wa maoni hayo unaweza kuwa wa aina nyingi ukiwa ni pamoja na kutuma ujumbe mfupi wa simu,majukwaa ya umma, tafiti, mijadala ya mitandao ya kijamii na mikutano ya kijamii.

“Kongamano hili ni kubwa na la kwanza kufanyika, hivyo uhamasishaji wa kongamano letu la maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 tunalojukumu la kutoa elimu juu ya Tanzania tuitakayo 2050 ili kuwaandaa vyema wananchi wote kutoa maoni yao ambayo yatachangia kwa asilimia 100 katika kuiandaa Dira 2050,”amesema Mafuru.

Amesema tume inatoa wito kwa wananchi wote kushiriki katika kutoa maoni yake kwa kutoa majibu kuhusu dira hiyo.

Amesisitiza kuwa maoni ya kila mtanzania yanathamani kubwa katika kuandaa dira hiyo hivyo ni vyema kwa kila mtu kushiriki ili kupata Dira itakayokidhi matarajio na mahitaji ya Taifa.

Aidha Mafuru amevitaka vyombo vya habari nchini kuripoti hatua zote za dira kwa kuandaa vipindi vya elimu na kuandaa mahojiano yatakayoendeshwa na tume ili kuongeza uelewa na ushiriki wa umma.

“Vyombo vya habari vinapaswa kuruhusu na kuunda njia kwa wananchi kueleza maoni yao katika vyombo vyenu waweze kuuliza maswali na kutoa maoni juu ya Dira 2050 tunaahidi tume tutafanya kazi kwa karibu na waandishi wa habari pamoja wadau wa maendeleo na mwananchi mmoja mmoja,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles