26.1 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko ameitaka wizara ya madini kukamilisha mpango wa mafuta na gesi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Kamishna wa mafuta na gesi kusimamia mpango wa mafuta na gesi ukamilike kwa haraka na kutumika ili kuendana na mpango wa matumizi bora ya nishati.

Agizo hilo amelitoa leo Alhamisi Mei 30,2024 Jijini hapa wakati wa uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya nishati,pamoja na matumizi ya magari yanayotumia umeme.

Naibu Waziri Mkuu, Dk.Biteko amesema mpango wa mafuta na gesi upo katika mchakato wa kukamilika, hivyo viongozi hao wanatakiwa kuharakisha mchakato huo ili uweze kukamilika na kuanza kutumika.

Aidha Naibu Waziri huyo amesema ni lazima mipango yote isomane ili kusilete sintofahamu yoyote katika utendaji huku akiitaka jamii kuendelea kuungana na Serikali katika juhudi mbalimbali za kutunza mazingira.

“Tuendelee kuungana na Serikali katika juhudi hizi nia yetu baada ya kuzindua kituo hicho tuone vituo vinazinduliwa katika maeneo mbalimbali,huko Mikoani”amesema Naibu Waziri Mkuu Biteko

Biteko amesema amefurahishwa na jinsi ambavyo Jumuiya ya Ulaya na UNDP zinavyoendelea kutoa misaada kwa Tanzania katika miradi mbalimbali.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru kwenye jambo hili kwa kuhakikisha watanzania wanapata nishati bora na yenye gharama ndogo,”amesema Biteko.

Mwakilishi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) ,Lamine Dialo amesema Umoja wa Ulaya utaendea kusaidia miradi mbalimbali inayohusu matumizi Bora ya nishati.

Naye,Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Shigeki Komatsubara amesema wataendelea kuhakikisha mazingira yanaendelea kutunzwa nchini kwa kusaidia miradi mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule amemshukuru Naibu Waziri Mkuu kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika kwani kwa Sasa hakuna changamoto yoyote huku akiwakaribisha wadau kutumia jua la Dodoma kuzalisha nishati ya umeme.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles